2TI_Kiswahili_1068.pdf

(42 KB) Pobierz
2Timotheo
Utangulizi
Paulo alikuwa amefungwa tena huko Rumi chini ya utawala wa Nero. Pengine huu ulikuwa waraka wa
mwisho kabisa wa Paulo. Baada ya kuandika waraka wake wa kwanza kwa Timotheo msaidizi wake, huenda
akiwa Makedonia, inaelekea Paulo alikamatwa aidha akiwa Troa au Nikopili (Tit.3:12) na kurudishwa gerezani
huko Rumi.
Katika waraka huu inakuwa kama vile Paulo anahisi fursa zake za kuhubiri Injili zinakaribia kikomo (4:6 – 8).
Ndani ya waraka huu wa binafsi Paulo anaeleza hisia zake za ndani kabisa. Anamkumbusha Timotheo kwamba
hata kama maisha yake hapa duniani yatakoma, Mungu alikuwa amemwandalia maisha ya milele (1:10-12).
Paulo pia anakumbusha juu ya uaminifu wa Mungu ambaye amemwongoza katika maisha yake yote. Anagusia
juu ya nyakati za hatari ambazo zingekuja, siku za taabu ambazo watu wataiacha kweli na kupenda anasa kuliko
kummpenda Mungu (3:1-8).
Wakati huu Paulo alikuwa mpweke na alitamani sana Timotheo aje aungane naye (4:9, 21). Anajitahidi
kumtia Timotheo moyo na kumwimarisha kwa ajili ya kazi kubwa aliyokabidhiwa. Paulo anatamani kumwona
Timotheo tena, akimwomba amletee vile vitabu vya ngozi alivyokuwa ameviacha Troa.
Anamwagiza Timotheo asimame imara katika mateso yajayo na kuilinda imani iliyo nyofu.
Wazo kuu
Barua hii inazungumzia hasa kuhusu uweza wa Mungu juu ya vitu vyote. Ingawa mateso yanakuja na
yataendelea kuongezeka, Mungu anatawala. Kwa hiyo wote wamwaminio haiwapasi kuogopa kitu cho chote.
Paulo anatoa ushuhuda wa imani yake, akieleza jinsi alivyopigana vita kwa ajili ya kweli na jinsi atakavyopewa
thawabu siku ya mwisho (4:6-8).
Tarehe
Waraka huu uliandikwa kati ya 66 – 67 B.K. wakati wa utawala wa Nero.
Mahali
Rumi.
Mgawanyo
Shukrani za Paulo kwa ajili ya Timotheo (1:1-5)
Maagizo ya Paulo kwa Timotheo (1:6-2:2)
Sifa za mtumishi mwaminifu (2:3-26 )
Mateso yajayo (3:1-17)
Maneno ya mwisho(4:1-22).
1
2Timotheo
16 Bwana akawahurumie watu wa nyumbani
mwa Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha
mara kwa mara wala hakuonea aibu minyororo
yangu. 17 Badala yake, alipokuwa Rumi,
alinitafuta kwa bidii mpaka akanipata. 18 Bwana
na amjalie kupata rehema kutoka kwa Bwana
siku ile! Nawe unajua vema jinsi alivyonisaidia
huko Efeso.
Salamu
Paulo mtume wa Kristo Yesu kwa
mapenzi ya Mungu, kulingana na ile ahadi
ya uzima uliomo ndani ya Kristo Yesu.
1
2 Kwa Timotheo, mwanangu mpendwa:
Neema, rehema na amani kutoka kwa
Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.
Askari Mwema Wa Kristo Yesu
Basi, wewe mwanangu, uwe hodari katika
neema iliyo ndani ya Kristo Yesu. 2 Nayo
mambo yale uliyonisikia nikiyasema mbele ya
mashahidi wengi, uwakabidhi watu waaminifu
watakaoweza kuwafundisha watu wengine vile
vile. 3 Vumilia taabu pamoja nasi kama askari
mwema wa Kristo Yesu. 4 Hakuna askari ye yote
ambaye akiwa vitani hujishughulisha na mambo
ya kawaida ya maisha haya kwa sababu nia
yake ni kumpendeza yule aliyemwandika awe
askari. 5 Vivyo hivyo, yeye ashindanaye katika
michezo hawezi kupewa tuzo ya ushindi
asiposhindana kulingana na kanuni za
mashindano. 6 Mkulima mwenye bidii ya kazi
ndiye anayestahili kuwa wa kwanza kupata
fungu la mavuno. 7 Fikiri sana kuhusu haya
nisemayo, kwa maana Mungu atakupa ufahamu
katika mambo hayo yote.
8 Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka kutoka
kwa wafu, Yeye aliye wa uzao wa Daudi. Hii
ndiyo Injili yangu, 9 ambayo kwayo ninateseka
hata kufikia hatua ya kufungwa minyororo kama
mhalifu. Lakini neno la Mungu halifungwi. 10 Kwa
hiyo ninavumilia mambo yote kwa ajili ya
wateule wa Mungu, kusudi wao nao wapate
wokovu ulio katika Kristo Yesu, pamoja na
utukufu wa milele.
2
Shukrani Na Kutiwa Moyo
3 Ninamshukuru Mungu, ninayemtumikia
kwa dhamiri safi, kama walivyofanya baba
zangu, ninapokukumbuka usiku na mchana
katika maombi yangu. 4 Nikiyakumbuka machozi
yako, ninatamani sana kukuona ili nipate kujawa
na furaha. 5 Nimekuwa nikiikumbuka imani yako
ya kweli, waliokuwa nayo bibi yako Loisi na
mama yako Eunike na ambayo mimi nina sadiki
sasa wewe nawe unayo. 6 Kwa sababu hii
nakukumbusha uchochee ile karama ya Mungu,
iliyowekwa ndani yako nilipokuwekea mikono
yangu. 7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga,
bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa
kiasi.
8 Kwa hiyo usione haya kushuhudia kuhusu
Bwana wetu, wala usinionee haya mimi niliye
mfungwa kwa ajili Yake, bali uishiriki pamoja
nami taabu ya Injili kwa kadiri ya nguvu ya
Mungu, 9 ambaye alituokoa na kutuita katika
mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu
mema bali kwa sababu ya kusudi Lake
mwenyewe na neema Yake. Neema hii tulipewa
katika Kristo Yesu kabla ya kuwako kwa
ulimwengu. 10 Lakini sasa imefunuliwa kwa
kudhihirishwa Kwake Mwokozi wetu, Kristo
Yesu, ambaye amebatilisha mauti na kuleta
uzima na kutokufa kwa njia ya Injili. 11 Nami
nimewekwa kuwa mhubiri, mtume na mwalimu
wa Injili hii. 12 Hii ndiyo sababu ninateseka
namna hii, lakini sioni haya kwa maana
ninamjua Yeye niliyemwamini na kusadiki ya
kuwa anaweza kukilinda kile nilichokiweka
amana Kwake hadi siku ile.
13 Shika kwa uthabiti kielelezo cha
mafundisho yenye uzima yale uliyoyasikia
kwangu pamoja na imani na upendo katika
Kristo Yesu. 14 Ilinde ile amana uliyokabidhiwa
kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu.
15 Unajua ya kuwa watu wote katika Asia
wameniacha, miongoni mwao wamo Filego na
Hermogene.
11 Hili ni neno la kuaminiwa:
Kwa maana kama tumekufa pamoja naye,
tutaishi pia pamoja naye.
12 Kama tukistahimili,
pia tutatawala pamoja naye.
Kama tukimkana Yeye,
naye atatukana sisi.
13 Kama tusipoamini,
Yeye hudumu kuwa mwaminifu,
kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.
Mfanyakazi Aliyekubaliwa na Mungu
14 Endelea kuwakumbusha mambo haya
ukiwaonya mbele za Bwana waache
kushindana kwa maneno ambayo hayana faida
2
952117994.002.png
 
2Timotheo
yo yote bali huwaangamiza tu wale
wanaoyasikia. 15 Jitahidi kujionyesha kwa Mungu
kuwa umekubaliwa na Yeye, mtenda kazi asiye
na sababu ya kuona aibu, ukilitumia kwa usahihi
neno la kweli. 16 Jiepushe na maneno mabaya,
yasiyo na maana, yasiyo ya utauwa, kwa maana
hayo huzidi kuwatosa watu katika kukosa
heshima kwa Mungu. 17 Mafundisho yao
yataenea kama kidonda kinachooza. Miongoni
mwao wamo Himenayo na Fileto 18 ambao
wameiacha kweli, wakisema kwamba ufufuo wa
wafu umekwisha kuwako na kupotosha baadhi
ya watu. 19 Lakini msingi wa Mungu ulio
mathubuti umesimama ukiwa na muhuri wenye
maandishi haya: ‘‘Bwana anawajua walio wake’’
tena, ‘‘Kila alitajaye jina la Bwana auche uovu.’’
20 Katika nyumba kubwa kuna vyombo si vya
dhahabu na fedha tu, bali pia vimo vyombo vya
miti na vya udongo, vingine kwa matumizi
maalum na vingine kwa matumizi ya kawaida.
21 Basi ikiwa mtu amejitakasa na kujitenga na
hayo niliyoyataja, atakuwa chombo maalum,
kilichotengwa na ambacho kinamfaa mwenye
nyumba, kikiwa tayari kwa kila kazi njema.
22 Zikimbie tamaa mbaya za ujana, ufuate
haki, imani, upendo na amani pamoja na wale
wamwitao Bwana kwa moyo safi. 23 Jiepushe na
mabishano ya kipumbavu na yasiyo na maana,
kwa kuwa wajua ya kwamba hayo huzaa
magomvi. 24 Tena haimpasi mtumishi wa Bwana
kuwa mgomvi, bali inampasa awe mwema kwa
kila mtu, awezaye kufundisha, tena mvumilivu.
25 Inampasa kuwaonya kwa upole wale
wanaopingana naye, kwa matumaini kwamba
Mungu atawajalia kutubu na kuijua kweli, 26 ili
fahamu zao ziwarudie tena, nao waponyoke
katika mtego wa Shetani ambaye amewateka
wapate kufanya mapenzi yake.
Mungu . Jiepushe na watu wa namna hiyo.
6 Miongoni mwao wamo wale wajiingizao
katika nyumba za watu na kuwachukua mateka
wanawake wajinga, waliolemewa na dhambi
zao na kuyumbishwa na aina zote za tamaa
mbaya. 7 Wakijifunza sikuzote lakini kamwe
wasiweze kufikia ujuzi wa kweli. 8 Kama vile
Yane na Yambre walivyopingana na Mose,
vivyo hivyo watu hawa hupingana na ile kweli.
Hawa ni watu wenye akili zilizopotoka, ambao
wamekataliwa kwa mambo ya imani. 9 Lakini
hawataendelea sana, kwa sababu upumbavu
wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama
ulivyokuwa dhahiri upumbavu wa hao watu
wawili.
Paulo Amwagiza Timotheo
10 Lakini wewe umeyajua mafundisho yangu,
mwenendo, makusudi, imani, uvumilivu,
upendo, ustahimilivu, 11 mateso na taabu. Yaani,
yale mambo yote yaliyonipata huko Antiokia,
Ikonio na Listra, mateso yote niliyostahimili,
lakini Bwana aliniokoa katika hayo yote.
12 Naam, ye yote anayetaka kuishi maisha ya
utauwa ndani ya Kristo Yesu atateswa. 13 Lakini
watu waovu na wadanganyaji watazidi kuwa
waovu, wakidanganya na kudanganyika. 14 Bali
wewe, udumu katika yale uliyojifunza na
kuyaamini kwa uthabiti, ukitambua ya kuwa
ulijifunza hayo kutoka kwa nani 15 na jinsi
ambavyo tangu utoto umeyajua Maandiko
matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha
upate wokovu kwa njia ya imani katika Kristo
Yesu. 16 Kila andiko, lililovuviwa na Mungu lafaa
kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa
yao, kuwaongoza na kuwafundisha katika haki
17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa
apate kutenda kila kazi njema.
Hatari Za Siku Za Mwisho
Lakini yakupasa ufahamu jambo hili,
kwamba siku za mwisho kutakuwa na
nyakati za hatari. 2 Kwa maana watu watakuwa
wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda
fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye
kumkufuru Mungu, wasiotii wazazi wao, wasio
na shukrani, wasio watakatifu, 3 wasio na
upendo, wasiopenda kupatanishwa,
wasingiziaji, wasiozuia tamaa zao, wakatili,
wasiopenda mema, 4 wasaliti, wakaidi, waliojaa
majivuno, wapendao anasa zaidi kuliko
kumpenda Mungu. 5 Wakiwa na mfano wa
utauwa kwa nje lakini wakizikana nguvu za
Maagizo Ya Mwisho
Nakuagiza mbele za Mungu na mbele za
Kristo Yesu, atakayewahukumu watu
walio hai na waliokufa wakati wa kuja Kwake na
ufalme Wake kwamba: 2 Uhubiri Neno, uwe
tayari wakati ufaao na wakati usiofaa, karipia,
kemea na kuonya kwa uvumilivu wote na kwa
mafundisho mazuri. 3 Maana wakati utakuja watu
watakapokataa kuyakubali mafundisho yenye
uzima, badala yake, ili kutimiza tamaa zao
wenyewe watajikusanyia idadi kubwa ya walimu
wapate kuwaambia yale ambayo masikio yao
yanayowasha yanatamani kuyasikia.
4 Watakataa kusikiliza kweli na kuzigeukia
3
4
3
952117994.003.png
 
2Timotheo
hadithi za uongo. 5 Kwa habari yako wewe,
vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Injili,
timiza wajibu wote wa huduma yako.
6 Kwa maana mimi sasa ni tayari kumiminwa
kama sadaka ya kinywaji, nayo saa yangu ya
kuondoka imetimia. 7 Nimevipiga vita vizuri,
mashindano nimeyamaliza, imani nimelinda.
8 Sasa nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana,
mwamuzi wa haki, atanitunukia siku ile, wala si
mimi tu, bali pia wote ambao wamengoja kwa
shauku kuja Kwake.
Maombi Ya Binafsi
9 Jitahidi kuja kwangu upesi 10 kwa sababu
Dema, kwa kuupenda ulimwengu, ameniacha
na amekwenda Thesalonike. Kreske
amekwenda Galatia na Tito amekwenda
Dalmatia. 11 Ni Luka peke yake ndiye aliye hapa
pamoja nami. Mtafute Marko uje naye kwa
sababu ananifaa sana katika huduma yangu.
12 Nimemtuma Tikiko Efeso. 13 Utakapokuja,
niletee lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa
na vile vitabu vyangu, hasa vile vya ngozi.
14 Aleksanda, yule mfua chuma alinitendea
ubaya mkubwa. Mungu atamlipa kwa ajili ya
yale aliyotenda. 15 Wewe pia ujihadhari naye kwa
sababu aliyapinga sana maneno yetu.
16 Katika utetezi wangu wa mara ya kwanza,
hakuna hata mmoja aliyeniunga mkono, bali kila
mmoja aliniacha. Namwomba Mungu
wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. 17 Lakini
Bwana alisimama upande wangu akanitia
nguvu, ili kwa kunipitia mimi lile Neno lihubiriwe
kwa ukamilifu, watu wote Mataifa wapate
kulisikia. Mimi niliokolewa kutoka katika kinywa
cha simba. 18 Bwana ataniokoa katika kila
shambulio baya na kunileta salama katika
Ufalme Wake wa mbinguni. Atukuzwe Yeye
milele na milele. Amen.
Salamu Za Mwisho
19 Wasalimu Prisila, Akila na wote wa
nyumbani kwa Onesiforo. 20 Erasto alibaki
Korintho. Nami nikamwacha Trofimo huko
Mileto akiwa mgonjwa. 21 Jitahidi ufike huku
kabla ya majira ya baridi. Eubulo anakusalimu,
vivyo hivyo Pude, Lino, Klaudia na ndugu wote.
22 Bwana awe pamoja na roho yako. Neema
iwe pamoja nanyi. Amen.
4
952117994.001.png
 
Zgłoś jeśli naruszono regulamin